Nandy adai hakufikiria kushinda tuzo ya Afrima

0
184

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amesema kuwa hakufikiria kama angeshinda tuzo ya Afrima nchini Nigeria kutokana na wasanii aliokuwa anashindanishwa nao.

Nandy amesema kuwa alikuwa aamini kama angeibuka na ushindi wa tuzo hiyo baada ya kuwekwa na wasanii wakongwe ambao walishakuwa maarufu maarufu kimataifa kuliko yeye ambaye ni kwanza anachipukia.

Msanii huyo amesema kuwa alikuwa na hofu mara baada ya kushindanishwa na wasanii ambao wameshamtangulia kufahamika kimataifa kama vile Vanessa Mdee , Juliana Kanyomozi na Victoria Kimani ambao wote walikuwa katika kipengele kimoja cha Best Female Eastern Africa.

Pia amesema kuwa wakati anatangazwa mshindi katika kipengele hicho aliamua kuziba masikio ili asisikie nani ndio mshindi lakini cha ajabu jina lake ndio akasikia linatajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo.

Mwanamuziki huyo kwasasa anaonekana kufanya vizuri kwa upande wa kinana kutokana na ubora wake kazi zake.

LEAVE A REPLY