Nana afungukia changamoto za kazi yake

0
33

Mrembo wa video za muziki, Nana amefunguka ugumu anaopitia katika sanaa yake ya kuigiza pamoja na video za wasanii wa Bongo Fleva.

Nana amesema kuwa anapata shida sana kuigiza kipande cha mapenzi katika kazi yoyote anayopata , kwani anajisikia huru kufanya hivyo na mume wake pekee.

“Napata ugumu kuigiza scene ya kuwa romantic kwasababu sijawahi kufanya hivyo na mwanaume mwingine yeyote tofauti  na mpenzi  wangu , inakuwa ngumu   sio rahisi ‘kukisi’ unajua eeh, au kuigiza kulia sio kitu rahisi,” alisema mrembo huyo .

Nana amesema kuwa mbali na kutopenda kuigiza mambo ya mapenzi, anafurahia sana kufanya kazi kwa ratiba na ushirikiano toka kwa wasanii wenzake.

LEAVE A REPLY