Naj amkingia kifua Baraka The Prince

0
68

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naj amemkingia kifua mpenzi wake ambaye ni msanii Barakah The Prince baada ya sasa hivi kubadilika.

Naj amesema sasa hivi amejitafuta na amebadilika kwa kutojibu watu vibaya katika mtandao wa Instagram.

Naj amesema hivyo baada ya kuwepo na taarifa juu ya kutajwa kwa mpenzi wake huyo, kwamba ndiye msanii anayeongoza  kuwajibu mbovu mashabiki mitandaoni.

“Kiukweli amelifanyia kazi hilo jambo, sidhani kama kipindi cha hapa karibuni amemjibu mtu vibaya kuna muda inatokea kama binadamu.

Pia kuna comments zinakukwaza sana hadi ukapoteza muelekeo, huyu sio Barakah yule ambaye mmemzoea kwamba kila kitu kinamkasirisha ndiyo maana amejitafuta kwenye hiyo miaka miwili”.

LEAVE A REPLY