Nai akiri kuachana na Moni Centrozone

0
128

Video vixen Bongo, Nai amefunguka na kukiri kuwa ameachana na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moni Centrozone.

Kauli ya video vixen huyo inakuja kufuatia kuulizwa maswali na baadhi ya mashabiki wake kuhusu mahusiano yao ambayo yalipa umaarufu kwenye sekta ya Sanaa hapa nchini toka walipoanza mahusiano hayo.

Nai amewataka watu waendelee kuongea, lakini hawezi kumrudia mwanamuziki huyo kutokana na tabia zake kuwa mbaya kwenye mahusiano yao.

Pia Nai amesema kuwa kuachana ni kawaida na mara kwa mara watu wamekuwa wakitabiri kuwa wataachana na sasa wameachana kweli.

“Kwa sasa tumeachana kweli na siwezi kurudiana na Moni japokuwa tumetoka mbali tangu tukiwa Dodoma. Kuachana ni kawaida, wanaachana watu wakiwa wamezaa watoto nane, itakuwa sisi hata mmoja atuna alisema mchezaji huyo.

Wawili hao kwasasa hawapo kwenye mahusiano baada ya kuachana lakini Nai amekanusha kuondoka na viu vyote baada ya kuachuana huku akisema kuwa yeye ameondoka na vitu vyake tu alivyonunua mwenyewe.

LEAVE A REPLY