Nai akanusha kuolewa

0
59

Video vixen Bongo, Nai amefunguka na kukanusha taarifa za kuolewa kama zilivyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Nai ameamua na kufafanua ukweli wa mambo baada ya kudaiwa kuwa amefunga ndoa kimya kimya jambo ambali amelikana vikali.

Nai alisema hajafunga ndoa kama watu wanavyodai, bali yeye ana saluni, hivyo kujilemba ni jambo la kawaida.

“Yaani wakiona umetupia picha tu, wanaanza kuijaji. Mimi nimepaka piko kama urembo, yaani nilikuwa naonyesha kazi yangu kwa sababu mimi najihusisha na urembo, maana nina saluni, basi wao ndio wakajua mimi nimeolewa.

Ni mapema mno mimi kuwa na mahusiano kwa kuwa nimetoka kuachana na Moni muda si mrefu, sasa hivi natafuta hela tu,” alisema Nai.

LEAVE A REPLY