Nahreel afunguka sababu ya Rosa Ree kuondoka The Industry

0
116

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka katika kundi la Navy Kenzo, Nahreel amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu msanii Rosa Ree kuondoka Kwenye label yake ya The Industry.

Rosa Ree alianza kujulikana baada ya kusainiwa chini ya label ya The Industry inayomilikiwa na Nahreel ambaye pia ni producer.

Rosa Ree alitangaza kuondoka kwenye label hiyo mapema mwaka jana baada ya kuwepo humo kwa muda mrefu huku akidai sababu pekee iliyomuondoa ni kuisha kwa mkataba wake na kusisitiza hana ubaya nao.

Rosa Ree aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo yalifanyika ndani ya label hiyo ambayo hayakumfurahisha ikiwemo kukataa kumpa akaunti yake ya Youtube hali iliyoashiria kulikuwa na kabifu fulani.

NAhreel anefunguka kwa mara ya kwanza na kumuongelea Rosa Ree tangu alipoondoka The Industry ambapo ameweka wazi hakukuwa na bifu baina yao bali mwenyewe aliomba kuondoka.

LEAVE A REPLY