Mzungu kichaa afanya ngoma na Fid Q

0
212

Msanii wa bongo fleva, Espen Sorensen ‘Mzungu Kichaa’ amesema katika albamu yake mpya ambaye anatarajia kuiachia hivi karibuni kuna nyimbo ambayo amewashirikisha Fid Q na King Kikii.

Mzungu Kichaa amesema mwanzoni alikuwa hazipi kipaumbele kolabo kwasababu alihitaji kutoka kimuziki mwenyewe.

“Ninatarajia kutoa albam yangu ya kwanza na katika nyimbo zilizomo ndani ipo ambayo nimefanya na Fid Q pamoja na King Kikii, hao ni wasanii ambao niliona kazi zao ambazo wamezifanya nikaridhika nazo ndio maana nilikubali kufanya nao kazi.

“Mwanzoni nilikuwa naona ugumu kufanya kolabo, wasanii kibao walikuwa wakinifuata ili nifanye nao kazi lakini sikuwa tayari, ila sasa nimekubali kufanya kolabo na yeyote yule,” alisema.

LEAVE A REPLY