Mzee Yusuf awataka wapenzi wa Taarab kufuta nyimbo zake

0
265

Aliyekuwa mwimbaji na Mkurugenzi wa bendi ya Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf amefunguka na kutilia mkazo na kuwaomba watu hususani wanawake ambao bado wana nyimbo zake za Taarab kwenye simu wazifute ili iwe kheri zaidi kwenye imani yake na dini yake.

Mzee Yusuf alisema hayo alipokwenda Babati mkoani Manyara katika harakati ya kuzidi kukutana na watu na kuwaomba wazifute nyimbo zake hizo za Taarab kwa kuwa anaamini zinakwenda kinyume na imani yake.

Mzee Yusuf amesema kuwa “Niko Babati kuzidi kuwaomba Waislam wanifanyie ‘Ihsaan’ ya kuzidi kuniombea dua na kuzifuta nyimbo zangu kwenye simu zao kwa ajili ya dini ya ‘Allah’ iwe kheri na salama. Wengine nyinyi mpaka sasa simu zenu bado zinabalaa naombeni mzifute kwa ajili ya ‘Allah’ naona haya simu zikipigwa zikaita hizo nyimbo kwani najisikia vibaya sijui nifanyaje”.

Aidha Mzee Yusuf alisema kuwa kwa sasa anaogopa na kuwataka wale ambao wanasema wamemkumbuka kwenye masuala ya uimbaji wa nyimbo za Taarabu waache kumkumbuka kwenye mambo hayo bali wamsaidie kwa kuzifuta nyimbo hizo. Mbali na hilo Mzee amewaomba watu wa vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii kufuta kazi zake zote hizo kwa ajili ya hisani ya ‘Allah’.

LEAVE A REPLY