Mzee Yusuf arejea rasmi kwenye Taarab

0
130

Mwanamuziki wa Taarab, Mzee Yusuf leo anatarajia kutoa burudani katika ukimbi wa Dar Live baada ya kurejea rasmi kwenye muziki huo.

Mzee Yusuf amesema, siku hiyo ndiyo mashabiki wake watajua alikuwa anamaanisha nini aliposema anarudi mjini.

Amesema amepokea maoni mengi kutoka kwa wadau tofauti na siku hiyo ataweka kila kitu wazi kuhusu uamuzi wake wa kurudi mjini.

Pia Mzee Yusuf amesema kuwa“Naomba mashabiki wangu wafike kwa wingi, kama mnavyojua huwa sinaga kazi mbovu mjini, mfalme narudi tena narudi kwa kishindo kikubwa, nimejipanga kuwapa burudani ya kutosha.

Shoo hiyo ilikuwa ifanyike Julai 31 mwaka huu, lakini kutokana na msiba mzito uliolikumba taifa wa kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini William Mkapa, ilisogezwa mbele.

Kabla ya kuacha kuimba Taarab, alikuwa tishio kwenye muziki huo ambapo ngoma zake kama Kaning’ang’ania, Mahaba Niue, Mpenzi Chocolate na Najiamini bado zinatamba mtaani mpaka sasa.

LEAVE A REPLY