Mzee Yusuf adai maisha yake yameyumba baada ya kuacha kuimba Taarab

0
1406

Aliyekuwa mmiliki wa band ya Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf amefunguka na kusema kuwa toka ameamua kuachana na biashara ya muziki na kumrudia Mungu maisha yake yameyumba.

Mzee Yusuf amebainisha hayo baada ya watu kutaka kujua je baada ya kuupa kisogo muziki wa taarabu maisha yake yapoje kwasasa.

Mzee Yusuf amesema kuwa licha ya uchumi wake kuporomoka lakini amekuwa na amani, furaha na maisha hayo kuliko kipindi cha nyuma kutokana na kumtumikia mungu kwasasa.

Mzee Yusuf amesema wakati anafanya kazi ya muziki alikuwa na maisha bora sana na kufanya vitu ambavyo anataka kufanya bila wasiwasi wowote tofauti na sasa ambapo akihitaji kitu fulani lazima ajipange kweli kweli ili kukipata.

Pia amesema kuwa ajutii maisha hayo kwani ni bora sana kwake kutokana na kumrudia mungu kwa kiasi kikubwa kuliko kipindi cha nyuma kwa hiyo haoni shida na maisha hayo.

Alipoulizwa kuhusu kuimba Qaswaida Mzee Yusuf amesema kuwa suala hilo lipo kwenye mipango yake ya baadae ila kwasasa babo.

Mzee Yusuf alitangaza kuachana na muziki wa Taarab mwaka jana na kumrudia mungu kwa kufanya ibada wakati wote mpaka kupelekea kwenda Macca kwa ajili ya kuhiji.

LEAVE A REPLY