Mzee Magali awataka wasanii wa Bongo Movie kujituma

0
37

Muigizaji wa Bongo Movie, Charles Magali amesema kuwa ameshangazwa na mastaa wakubwa wa filamu hapa nchini kugalagazwa na watoto katika Tuzo za Sinema Zetu.

Mzee Magali amesema wasanii waache kubweteka na ustaa wao na kusahau kujituma maana wasanii wanaochipukia wanakuja kwa kasi na wakizidi kubweteka wataendelea kulialia kuonewa kila kukicha.

“Nimesikia tuzo kubwa kama ya Msanii Bora wa Kiume na Msanii Bora wa Kike imekwenda kwa watoto hao ambao walikuwa hawajulikani, kwa kweli mastaa wanatakiwa kujiongeza na si kuishia kuwalaumu waandaaji.

Mkali huyo anayetisha kwa uigizaji wa kibabe, hivi karibuni anatarajia kurudi nchini na kuweka mikakati ya kuiinua tasnia hiyo.

LEAVE A REPLY