Mwili wa mama yake P Funk kuzikwa Uholanzi

0
37

Mwili wa mama mzazi wa mtayrishaji wa muziki wa Bongo Fleva P Funk Majani, Aunt Sheilah utazikwa leo nchini Uholanzi kutokana na kushindikana kurejea nchini kwasababu ya changamoto za usafiri.

Mwenyekiti wa kamati wa maandalizi wa msiba huo ambaye ni msanii Soggydogg amesema mwili utazikwa Uholanzi na P Funk mwenyewe yupo huko kwa ajili ya mazishi, ambapo  atarejea Tanzania Ijumaa usiku na siku ya Jumamosi watafanya dua maalum kwa marehemu.

“Siku ya leo tunarajia mwili wa mama mzazi wa P Funk Majani Aunt Sheilah kuzikwa nchini Uholanzi, imebidi azikwe huko kwa sababu usafiri ulikuwa mgumu na wenzetu bado wana wasiwasi na ugonjwa wa Corona.

 P Funk Majani mwenyewe tayari yupo huko kwa ajili ya mazishi na atarejea Tanzania siku ya Ijumaa usiku, kisha Jumamosi itafanyika dua ya marehemu nyumbani kwake Bamaga mahali ambapo ipo studio za Bongo Records”.

Mama wa P Funk Majani alifariki nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu siku ya Septemba 8, na taarifa kuhusu kifo chake zilitoka Tanzania siku ya Septemba 10.

LEAVE A REPLY