Mwenyekiti wa UVCCM Taifa afanya mazungumzo na viongozi wa UVCCM Dar

0
318

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James jana amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya utekelezaji ya mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa baraza la vijana wilaya ya Kinondoni.

Pamoja na mambo mengine mwenyekiti amesisitiza kuwa nguvu ya vijana wa CCM itumike vizuri katika kuhakikisha inashinda uchaguzi mdogo ujao wa jimbo la Kinondoni.

Baadhi ya wajumbe wa Vyuo na Vyuo vikuu waliohudhuria mkutano huo wa mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James
Baadhi ya wajumbe wa Vyuo na Vyuo vikuu waliohudhuria mkutano huo wa mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James

Wakati huo huo mwenyekiti huyo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa seneti ya Vyuo vikuu vilivyopo mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wa matawi ya vyuo hivyo.

Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na kaimu katibu mkuu wa Umoja huo taifa Shaka Hamdu Shaka, mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Asha Feruz pamoja na mjumbe wa Baraza kuu taifa Alex Gwantwa.

LEAVE A REPLY