Mwasiti amwagia sifa Nandy

0
34

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi amemwagia sifa mwanamuziki mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ akisema ni mpambanaji kwelikweli.

Mwasiti anasema kuwa, tangu mwanzo alikuwa akiwaambia watu kwamba Nandy lazima atafanikiwa.

Amesema kuwa “Nilisema tangu muda mrefu; Nandy ni mpiganaji hata ukifutalia kwenye mahojiano yangu hapo nyuma nilikuwa nawaambia watu lazima atakuja kufanikiwa kutokana na jinsi anavyojituma, leo utabiri wangu umetimia,”.

Nandy ni mwanamuziki anayefanya vizuri kwasasa kutokana na ubora wa nyimbo zake ambapo kwasasa anatamba na kibao alichomshirikisha mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide.

LEAVE A REPLY