Mwasiti afunguka ukaribu wake na Godzilla

0
138

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi ameweka wazi kuwa alishawahi kufuatwa na mama mzazi wa marehemu Godzilla akimtaka amsaidie, ili naye afanikiwe.

Mwasiti amesema kwamba kutokana na jambo hilo akawa karibu sana na familia ya Godzilla, na kushirikiana kwenye masuala mbali mbali.

Msanii huyo amesema kuwa “Ilikuwa benki mjini, Godzilla alikuwa amekuja na mama yake, akaniambia napenda unavyoimba, ningependa pia umshike mkono mdogo wako na yeye aishi katika mazingira mazuri na kufanya kazi.

Mwasiti ni mmoja wa watu ambao walikuwa karibu sana na Godzilla, na kuweza kufanya kazi pamoja huku wakiwa na mlengo ya kuachia album ya pamoja.

Godzilla amefariki dunia juzi Februari 13, na anatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi, Februari 16 katika makaburi ya Kinondoni.

LEAVE A REPLY