Mwarabu Fighter apata ajali mbaya

0
515

Mlinzi wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Mwarabu Fighter amedai kuwa amepata ajali mbaya iliyosababisha kupasuka kichwani na kukimbizwa katika Hospitali ya Lugalo iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwarabu kupitia akaunti yake ya Instagrama amewashukuru madaktari wa Lugalo kwa huduma ya kwanza lakini hakueleza ajali hiyo imetokea lini, wapi na ilikuwaje, tutaendelea kukujuza kuhsu undani wa tukio hilo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Ndugu zangu nimepata ajali mbaya sana nimepasuka kichwani ila ninawashukuru Lugalo Hosptal kwa kunipatia huduma ya kwanza sasa hivi wananikimbiza Muhimbili kwa hiyo dua zenu ndugu zangu,”.

LEAVE A REPLY