Mwanzo wa mwisho wa ushkaji wa Majani na Chameleone unaanzia hapa?

0
387

Unaikumbuka ngoma ya Profesa Jay ‘NIKUSAIDIEJE’? Ni ngoma ambayo kutokana na kutisha kwake ilipelekea staa wa Uganda Jose Chameleone naye kuiomba beat hiyo na kutoka na ngoma BOMBOCLAT.

Kilichomvutia sana staa huyo wa Uganda ilikuwa ni beat ya ngoma hiyo ambayo iliandaliwa na producer mkongwe na bora, Majani a.k.a Khalfan a.k.a P.

Tatizo ni kuwa staa huyo wa Uganda hakumaliza malipo ya beat hiyo kwa majani hivyo beat hiyo ni mali halali ya Majani lakini kama hilo halitoshi staa wa Uganda Jose Chameleone anadaiwa kumpiga chenga ya mwili majani na kuvuta mkwanja mrefu kwa kukubali beat hiyo itumike kwenye movie ya QUEEN OF KATWE.

Kwa mujibu wa Majani, staa huyo wa Uganda anadai kulipwa $2,000 kitu ambacho Majani haamini na kinachomtia shaka zaidi ni kitendo cha Chameleone kuwa kimya katika kila hatua ya kuuza beat hiyo hadi Majani alipokuja kustuka na kudai ‘haki’ yake.

Ngoma hii kwa sasa imefikishwa kwa watayarishaji wa movie hiyo, Walt Disney ambao wamekubali kumalizana na Majani.

Hatma ya mgogoro huu kuwavuruga Majani na Chameleone?

LEAVE A REPLY