Mwanzo wa mwisho wa Demba Ba? Avunjika vibaya mguu wa kushoto

0
463

Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle United na Chelsea za Uingereza, Demba Ba amevunjika vibaya mguu wa kushoto wakati anaichezea timu yake ya sasa ya Shanghai Shenhua kwenye ligi ya China maarufu kama Chinese Super League.

Demba Ba aliangua wakati akiwania mpira na mlinzi, Sun Xiang wa timu ya Shanghai SIPG Jumapili.

Kocha wa timu ya Shanghai Shenhua Gregorio Manzano amekaririwa akisema kuwa hofu yake kubwa ni kuwa huenda tukio hilo likamaliza maisha ya soka ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Newcastle United.

Mechi hiyo ilimalizika kwa Shanghai Shanhua kuwafunga wapinzani wao wa jadi, Shanghai SIPG kwa mabao 2-1.

Ba mwenye miaka 31 ndiye kinara wa magoli kwenye ligi hiyo akiwa na magoli 14 kutokana na mechi 18 alizocheza tangua ajiunge na ligi ya China akitokea besiktas ya Uturuki mwaka 2015.

Tayari klabu yake ya zamani ya Chelsea imetuma salamu za pole na kumtakia heri ya kupona haraka.

Pole: Mshambuliaji wa Shanghai Shenhua Demba Ba

Pole: Mshambuliaji wa Shanghai Shenhua Demba Ba

LEAVE A REPLY