Mwandishi mahiri Pavel Sheremet auawa Urusi

0
132

Mwandishi maarufu wa habari wa Belarus, Pavel Sheremet ambaye alikuwa akifanyia kazi zake nchini Ukraine amefariki dunia baada ya gari yake kulipuka kwenye mji wa Kiev nchini Urusi.

Mwandishi huyo wa habari ambaye aliwahi kufanya kazi na televisheni ya taifa ya Urusi kabla ya kuhamia nchini Ukraine anadaiwa kukutwa na masahibu hayo wakati akielekea kwenye kituo binafsi cha redio cha Vesti ambapo alikuwa anaendesha kipindi cha matangazo ya asubuhi.

Mlipuko huo unadaiwa kusababishwa na kitu kilichotegwa kwenye gari aliyokuwa akiitumia wakati akielekea kazini.

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko ameyaita mauaji hayo kuwa ni ukatili mkubwa na ameagiza uchunguzi wa haraka sana ufanyike juu ya tukio hilo.

Picha za video kutoka katika kamera za eneo hilo zinaonyesha gari ya mwandishi huyo likiwa na moshi mwingi na moto huku watu wakikimbilia kwenye eneo hilo kwaajili ya kuwasaidia majeruhi ndani ya gari hilo.

Sheremet alikuwa mtu pekee ndani ya gari hilo kwa wakati huo.

Rais Poroshenko ameviomba vyombo vya usalama vya washirika ikiwemo FBI na wataalamu wa Umoja wa Ulaya kusaidia kwenye uchunguzi huo.

Sheremet alikuwa mwandishi mwenye wasifu mkubwa na alishawahi kufungwa jela na kuvuliwa uraia wa Belarus kwa kuripoti dhidi ya serikali ya rais Alexander Lukashenko mwaka 1997.

Shemeret pia aliwahi kuripoti vikali dhidi ya viongozi wa Ukraine na Urusi hivyo kifo chake kimezua maswali mengi huku ikidhaniwa kuwa huenda alikuwa akiwindwa kwa muda mrefu.

Mlipuko: Gari aliyokuwepo marehemu Sheremet baada ya kulipa
Mlipuko: Maafisa usalama wakiichunguza gari aliyokuwepo marehemu Sheremet baada ya kulipa

LEAVE A REPLY