Mwanamuziki wa Marekani auawa kwa kupigwa risasi

0
86

Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Nipsey Hussle ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa dukani kwake jijini Califonia nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali na vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti juu ya kifo cha rapa Nipsey Hussle aliyepigwa Risasi mbele ya duka lake la Mavazi Marathon Clothing.

Maafisa wa usalama wamesema kuwa Nipsey alishambuliwa na Risasi kadhaa mwilini mwake na Alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospital.

Jina kamili la Nipsey ni Ermias Davidson Asghedom alikulia Los Angels na miaka ya 90 alijihusisha na makundi kadhaa ya Uhalifu nchini humo.

Polisi nchini Marekani bado haijatoa ripoti kamili juu ya mauaji hayo kama yalikuwa ya kulipiza kisasi jijini humo.

LEAVE A REPLY