Mwanamuziki wa Kenya amponda Zari kurudiana na Diamond

0
1647

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka Kenya Ringtone Apoko amemjia juu Zari baada ya kuanza kusikika kwa tetesi kuwa amerudiana na Diamond.

Ringtone alikiri kumpenda Zari na kudai yupo tayari kumuoa na hata kumnunulia gari aina ya Range Rover mpya ambayo Zari aliikataa.

Lakini sasa Ringtone amerudi kumhoji Zari kuhusu Tetesi za yeye kurudiana man Diamond Ikiwa alishatangaza kuwa wameachana na hawezi kurudi kwake Tena.

Siku ya jana kuna Tetesi zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Zari na Baby dady wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz wamerudiana baada ya kutengana kwa takribani Miezi minne.

Ringtone amemtolea povu Zari kwa uamuzi wake wa kuamua kupasha kiporo na Diamond ambapo amempa ushauri wa kutorudiana na Diamond.

LEAVE A REPLY