Mwanamuziki wa Bongo fleva aacha muziki

0
126

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jolie ambaye amewahi kupitia THT na kufanya kazi na Petitman kama meneja wake ametangaza rasmi kuacha kazi ya muziki.

Jolie hakusema sababu yay eye kuacha muziki ambao aliufanya zaidi ya miaka mitatu na kufanikiwa kuachia vibao kadhaa na jina lake kuanza kujulikana rasmi kwenye medani ya muziki.

“Nani anaweza kufananisha hivi, nimefanya muziki na ninaacha,” ameandika msanii huyo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram pia mrembo huyo amewahi kuachia kazi kama vile “Bado, Uoga ,Sina na Haimaanishi.

Jolie sio msanii wa kwanza Bongo, kutangaza kuacha kazi ya muziki hivyo anaingia kwenye kitabu ambacho Vanessa Mdee yupo ndani yake.

LEAVE A REPLY