Mwana FA na Babu Tale wakutana na katibu mkuu wa Habari na Sanaa

0
62

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA na Babu Tale wamekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi kwa mazungumzo jijini Dodoma.

Babu Tale na Mwana FA ambao ni miongoni mwa wabunge kadhaa wanaojihususha na shughuli za sanaa, walikutana na Dkt. Abbasi Novemba 14 2020.

Lengo kuu la kukutana na katibu mkuu huyo wa wizara ya Habari ni kuzungumzia sekta ya Sanaa ambayo wawili hao ndiyo wanapotokea kabla ya kuwa wabunge.

Babu Tale ni mbunge anayewakilisha Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki na Mwana FA ni mbunge anayewakilisha jimbo la Muheza Tanga wakiwa ni wabunge wapya katika Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

LEAVE A REPLY