Mwana FA ataka adhabu ya Diamond na Rayvanny ipunguzwe

0
121

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA ameiomba Basata ipunguze adhabu waliyopewa wanamuziki Rayvanny na Diamond Platnumz kutokana na wimbo wao wa ‘Mwanza’.

Mwana FA ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ameomba adhabu waliyopewa wanamuziki hao ipunguzwe  au ifutwe ili kutowaumiza wasanii hao.

Mwana FA ametoa wito huo leo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea ofisi za Basata siku ya jana.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa jukumu la kufungia wimbo si lake na yeye alichofanya ni kwenda kujaribu kuongea na kuwaomba watendaji kwamba adhabu watakayoichukua isiwaumize moja kwa moja wasanii hao hata kama kuna makosa yamefanyika.

Amesema kuwa uongozi mzima wa Wasafi Classic Baby (WCB) na wasanii wao wanapaswa kuandika barua ya kuomba radhi na kuomba kupunguziwa adhabu, halafu hao kama watendaji ndiyo wataamua la kufanya lakini la msingi naamini adhabu haitabaki kama ilivyotolewa siku ya jana.

LEAVE A REPLY