Mwana FA afunguka kukutana na Mourinho

0
392

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amefunguka kwa kusema kuwa amejisikia faraja baada ya kukutana na aliyekuwa kocha wa timu Manchester United, Jose Mourinho.

Mwana FA alikutana na kocha huyo wa zamani wa United na kupata bahati ya kupiga picha na mreno huyo mwenye mbwembwe nyingi katika kazi yake ya ukocha.

Mwana FA akishuhudia mechi ya Manchester United dhidi ya West Ham uwanja wa Old Trafford
Mwana FA akishuhudia mechi ya Manchester United dhidi ya West Ham uwanja wa Old Trafford

Siku ya Jumamosi Mwana FA pia alipata nafasi ya kushuhudia mechi katika ya Manchester United dhidi ya West Ham United ambapo Manchester United waliibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Mwana FA ameshare picha akiwa na Mourinho wakiwa wamekaa kwenye viti na kuandika haya maeneno kwenye akaunti yake.

”Mara paaap,chuma hiki hapa..nikifute kazi tena?😂..no man natania ,nilifurahi kukutana na Jose Mourinho leo..yale maneno mabaya yote nikayaficha,nikamshukuru kwa nyakati nzuri alipokuwa kwetu na kumtakia bahati njema popote anapokwenda..na kuwa mimi ni mshabiki wake mkubwa,hasa anapoanza kuchonga..i feel good kukutana na this great man!

LEAVE A REPLY