Mwakyembe atangazwa mgeni rasmi mechi ya Yanga na Township Rollers

0
147

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe leo anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Township Rollers FC.

Taarifa hiyo imetolewa na msemaji wa klabu hiyo Dismas imeeleza kuwa Waziri Mwakyembe ndiye ataongoza maelfu ya mashabiki wa soka nchini watakaojitokeza kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange huo.

Taarifa hiyo imesema kuwa “Kwenye mchezo wa leo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC toka Botswa mgeni rasmi atakuwa Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe”.

Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na kati katika dimba la Taifa na baada ya wiki moja timu ya Yanga itaradhimika kusafiri kwenda nchini Botswana kwa ajili ya mechi ya marudiano.

LEAVE A REPLY