Mwakyembe afunguka tofauti ya Diamond na Alikiba

0
303

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa kama mvutano wa Diamond na Alikiba ni kiushindani hakuna haja ya kuwasuluisha.

Kauli hiyo ya Mwakyembe inakuja kufuatia siku za hivi karibuni kutokea mvutano mkubwa kati ya wawili hao.

Mwakyembe amesema haamini kama tatizo ni kubwa kiivyo bali ni kitu chenye afya tu kwa sababu kinaleta ushindani mzuri ambao unapeleka muziki katika ngazi nyingine.

Mwakyembe amesema kuwa “Kama kuna ushindani kati ya Alikiba na Diamond ambao ni kiuweledi, kitaaluma basi mimi nafikirii tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha, waendelee kushindani vizuri tupate miziki mizito,”.

Pia Dkt. Mwakyembe ameendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwaita pamoja Diamond na Alikiba ili kufanya ngoma pamoja kama alivyowahi kuhaidi hapo awali.

LEAVE A REPLY