Mvua yasababisha kifo cha mtu mmoja jijini Dar es Salaam

0
499

Mvua kubwa ilionyesha leo jijini Dar es Salaam imesababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo.

Maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo ni Jangwani pamoja na maeneo ya Bunguruni kwa Manyamani ambapo wakazi wa maeneo hayo wamehama kwa muda maeneo hayo kutokana na mafuriko hayo.

Maeneo ya Jangwani baada ya mafuriko
Maeneo ya Jangwani baada ya mafuriko

Katika eneo la Jangwani kumetokea kifo cha mtu mmoja ambaye amesombwa na maji ya mafuriko hayo wakati akiokota makopo maeneo hayo ya Jangwani.

Wakazi wa Jangwani wakitoka ndani ya nyumba zao kutokana na mafuriko hayo
Wakazi wa Jangwani wakitoka ndani ya nyumba zao kutokana na mafuriko hayo

LEAVE A REPLY