Muziki ulivyovunja ndoa ya Stamina

0
886

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Stamina amefunguka na kusema kuwa mambo aliyopitia kwenye ndoa yake na mke wake ndiyo sababu ya kuachia wimbo wake mpya ‘Asiwaze’.

Baada ya wimbo huo kumeibuka ishu kibao ikiwemo kusalitiwa na mkewe ambaye ndoa yao ilifungwa Mwezi Mei, 2018 mjini Morogoro na kutawaliwa na shamrashamra kama zote.

Stamina anayeunda Kundi la Rostam akiwa na Roma Mkatoliki amekiri muziki na simu kuwa chanzo kikubwa cha kuvunjika kwa ndoa yake kutokana na muda mwingi kuutumia studio.

“Muziki kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha mtafaruku uliosababisha mimi na mke wangu tutengane kwa sababu kuna muda nakuwa studio mpaka saa 8:00 usiku, kiasi kwamba nasinzia, nikija kushtuka saa 12:00 alfajiri na nikiangalia simu nakuta missed calls zaidi ya kumi.

“Pia muda mwingine ninapokuwa kwenye shoo kawaida tu siwezi kupanda na simu stejini, lakini utakuta mke anakosa imani na mimi na ugomvi unaanzia hapo,” anafunguka Stamina.

Stamina amefunguka mengi, ungana naye hapa chini ujue kinagaubaga kuhusiana na muziki wake pamoja na ishu ya ndoa yake kuvunjika’.

LEAVE A REPLY