Museveni apinga zuio la uingizwaji silaha nchini Sudan Kusini

0
98

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameilipinga pendekezo la Umoja wa Mataifa la kuzuia uingizwaji wa silaha kwenye nchi ya Sudan Kusini, na kudai hali hiyo italidhoofisha jeshi la nchi hiyo linaloendelea kupambana na waasi na kudhibiti hali ya mauaji inayojitokeza mara kwa mara nchini humo.

Akiwa kwenye mkutano wa nchi za Afrika uliofanyika jijini Kigali nchini Rwanda, rais Museven alisema, ‘Unapoweka sheria ya kutokuingizwa kwa silaha Sudan Kusini unadhoofisha uwezo wa jeshi la nchi hiyo ambapo utahitaji kujenga jeshi imara la muungano’.

Rais Museveni ameshatuma jeshi la nchi yake mara mbili kusaidia mapambano kwa kumuunga mkono rais wa nchi hiyo, Salva Kiir.

Sudan Kusini imeshashuhudia vifo vya zaidi ya watu 300 kwenye mapigano ya hivi karibuni ya nchini humo ambapo majeshi yanayoongozwa na serikali ya Kiir yamekuwa yakipambana na majeshi yanayomtii makamu wa rais, Riek Machar.

LEAVE A REPLY