Mume wa Queen Darleen aweka wazi anavyoishi wa wake zake

0
36

Mume wa mwanamziki Queen Darleen, aitwaye Isihaka ametolea ufafanuzi suala la yeye kumpendelea mke mdogo (Darleen)  na kutomjali mke wake mkubwa anayefahamika kama Sabra.

Amesema siyo kwamba kweli anampendelea mke wake mdogo kama inavyosemekana mtandaoni ila kwa kuwa Queen ni msanii; akipost kitu kinaenda sana kuliko mke mkubwa.

Pia mke mkubwa ana vitu vingi kuliko mke mdogo kwa sababu ana magari lakini Queen hajamnunulia na mke mkubwa ana nyumba yake lakini mke mdogo amepanga.

“Sabra ndiyo ana siku nyingi za kuwa na mimi, ana siku nne, halafu Queen Darleen ana siku tatu za kuwa na mimi,” amesema Isihaka.

LEAVE A REPLY