Muigizaji wa Bongo Movie afariki dunia

0
39

Muigizaji na Mshehereshaji Gladys Lawrance Chiduo maarufu kama MC Zipompa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 10, katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo Tegeta Jijini Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Chama cha Washehereshaji Tanzania, inaeleza kuwa chanzo cha kifo chake ni kuzidiwa kwa maradhi ya ghafla akiwa nyumbani kwake Mbweni Dar Es Salaam, kisha akakimbizwa kwenye Hospitali hiyo ili kuokoa maisha yake.

MC Zipompa alijiunga na chama hicho mnamo Septemba 3, 2001 akiwa kama ni miongoni mwa wanachama na waanzilishi wa chama cha washehereshaji Tanzania.

Aidha taarifa hiyo imesema taarifa hizo za msiba ni za awali hivyo taarifa kamili ya msiba ulipo, rambirambi na taratibu za mazishi zitatolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho na kamati ya dharura.

 

LEAVE A REPLY