Muigizaji mkongwe wa Marekani afariki dunia

0
440

Mastaa mbali mbali wa Hollywood kupitia mitandao ya kijamii wametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha muigizaji, muongozaji na mtunzi wa filamu nchini  Marekani, Garry Marshall aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Marshall amefariki jana akiwa hospitali mjini Burbank, California nchini Marekani ambapo alilazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.

Muigizaji mkongwe na muongoza filamu wa Marekani, Henry Winkler, ambaye aliigiza kwenye kipindi cha TV ‘Happy Days’ kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika “Rest In Peace Garry Marshall”.

Waigizaji wengine waliotoa salamu zao za rambi rambi ni Ashton Kutcher na Jessica Alba wote waliwahi kufanya kazi na Garry Marshall kwenye filamu ya Valentine’s Day, ambapo Alba kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika “True Pioneer Rest In Peace”.

LEAVE A REPLY