Mtulia ‘uso kwa uso’ na Salim Mwalimu leo

0
188

Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Maulid Mtulia leo amekutana uso kwa uso na mgombea wa Chadema, Salum Mwalim.

Wawili hao wamekutana kwenye mahojiano ya kipindi cha Africa Breakfast kinachorushwa na kituo cha Radio cha East Africa Radio.

Katika mahojiano yao Salim Mwalim alisema kuwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 alimpigania Mtulia ili ashinde ubunge jimbo la Kinondoni jambo ambalo mtulia amelipinga vikali.

Salim Mwalim almuuliza Mtulia anajisikia vipi baada ya kuwasaliti wana kinondoni ambao,  baadhi yao walipoteza maisha yao  wengine kubaki vilema na hata wajawazito kupoteza mimba zao wakati wakishinikiza Mtulia atangaziwe mshindi 2015.

Mtulia amesema kwamba, Mwalimu kumuambia kwamba alimpigania si kweli  kwani wakati wakati wa uchaguzi 2015, Mwalimu alikuwa anampigania mgombea mwingine wa jimbo la kikwajuni hivyo ana uhakika kwamba Mwalimu hakumpigania.

Mtulia mwaka 2015 alishinda uchaguzi wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CUF ambayo ilikuwa chini ya mwamvuli wa UKAWA unaounganisha vyama vinne vikiwepo, CHADEMA, CUF, NCCR na NLD.

 

LEAVE A REPLY