Mtoto arudisha penzi la Alikiba na mke wake

0
269

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba na mkewe Amina Khalef wamesheherekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao Keyaan iliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

Katika mitandao kulikuwa na madai mengi kwamba ndoa hiyo imeota mbawa kabla ya hivi karibuni wawili hao kuonekana wakiwa pamoja wakati mtoto wao Keenan akitimiza umri wa mwaka mmoja.

Mdogo wake na Alikiba aitwae Zabibu amesema kuwa anawashangaa kinoma watu walivyomuona kaka yake na mkewe huyo, wakaanza kusema kuwa kumbe hawajaachana.

Zabibu ni mke wa mchezaji wa kulipwa wa Tanzania anayekipiga Klabu ya Highland Park inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Abdi Banda amesema kuwa anafurahi sana kuwaona wanapendana.

Zabibu alisema kwenye ndoa hakukosekani changamoto, lakini kikubwa ni kuzikabili na maisha yaendelee. “Mimi ninawaombea sana siku zote wadumu miaka mingi zaidi maana changamoto zipo siku zote.

Mwaka jana kuliibuka tetesi nyingi mitandaoni juu ya kuvunjika kwa ndoa ya Kiba, lakini sasa mambo yametulia, wawili hao wanaendelea na maisha wakiwa wamejaaliwa mtoto huyo mmoja wa kiume.

LEAVE A REPLY