Mtatiro: Bora kushirikiana na CCM kuliko Profesa Lipumba

0
144

Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amefunguka na kujibu hoja za baadhi ya watu ambao wanataka CUF kukubaliana na Professa Lipumba kwa kuwa Mwenyekiti huyo ameshika makali kutokana na vyombo mbalimbali vya serikali kumtambua.

Julius Mtatiro ambaye sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kimasomo amesema hilo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema ni jambo ambalo halitawezekana wao kukubali yaishe na Profesa Lipumba na kusema wataendelea na harakati zao kuhakikisha haki yao inapatikana.

Mtatiro ameandika “Nasoma maoni ya baadhi ya watanzania kuja kwetu, kwamba kwa sababu serikali, dola, CCM, polisi, bunge, NEC, RITA, na Msajili wa Vyama vya Siasa wameshikamana kumuunga mkono Lipumba, na kwa hiyo ati Lipumba ameshikilia mpini na chama kimeshikilia makali kwa nini tusikubali yaishe? Lipumba apewe kila kitu…hadi roho zetu, lakini misingi yetu, misimamo yetu, umoja wetu na mshikamano wetu, hawezi kupewa. Hizi ndizo silaha zetu na niwaambie kuwa zina faida ya muda mrefu kuliko zile anazozitizama msaliti”.

Aidha Mtatiro anasema kuwa ni rahisi sana wao kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Profesa Lipumba

Pia ameandika kuwa “Ni mara kumi kumsamehe jirani yako aliyembaka mwanao, kuliko kumsamehe baba yako mzazi aliyembaka mwanao. Adui wa ndani, ni hatari zaidi kuliko adui wa nje. CCM ni adui bora kuliko Lipumba na kwa hiyo ni rahisi sana kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Lipumba”.

LEAVE A REPLY