Mshindi wa BSS afunguka matumizi ya pesa zake

0
60

Mshindi wa Bongo Star Search (BSS), Meshack Fukuta amesema kuwa akipata fedha zake za ushindi ambazo ni milioni 20 atazitumia kwa ajili ya muziki wake.

Meshack amesema kuwa fedha hizo sio nyingi wala kidogo, lakini asipotuliza akili anaweza kuja kujikuta amezitumia bila ya kutimiza malengo yake.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Sijapata fedha bado na ni lazima nijipange ili nisije kuchanganyikiwa, natarajia kupata mililioni 20 huku milioni 30 zikiingia moja kwa moja kwenye usimamizi wa kazi zangu”.

Aliongezea kuwa licha ya BSS kuwekeza Milioni 30 kupitia muziki wake kama mkataba wao unavyoeleza ila na yeye ameona ni bora kuwekeza fedha hizo kwa ajili ya muziki ili kutimiza malengo yake.

LEAVE A REPLY