Msemaji wa maveterani wa vita Zimbabwe, Douglas Mahiya akamatwa

0
140

Polisi nchini Zimbabwe wamemkamata msemaji wa maveterani wa vita Douglas Mahiya kufuatia maandamano na tangazo la kutomuunga mkono rais Mugabe.

Bw. Mahiya aliwekwa kizuizini Jumatano siku ambayo rais Mugabe alitishia kuwaadhibu maveterani wa vita ambao wiki iliyopita walitangaza kuvunja uhusiano wa kijamaa na kiongozi huyo.

Bw. Mahiya pamoja na watu wengine 150 wanaodaiwa kuwa wanachama wa Umoja huo wa maveterani wa vita walihudhuria mkutano wa chama hicho na kuja na tangazo rasmi la kumpinga rais Mugabe na kusitisha ushirika wao kwake na kumtuhumu kwa uongozi mbovu.

Wanasheria wa Zimbabwe wanaofanya kazi na shirika la haki za binadamu wanadai kuwa huenda Bw. Mahiya akashtakiwa kwa makosa ya kuidharau serikali na kuitukana ofisi ya rais.

Mpaka kufikia jana jioni mashtaka rasmi ya Bw. Mahiya yalikuwa hayajatangazwa.

Inadaiwa kuwa mapema juzi polisi wa Zimbabwe waliivamia nyumba ya Mahiya kwa lengo la kumkamata lakini hakuwepo na baadae alijisalimisha polisi.

LEAVE A REPLY