Msechu akanusha kufulia kimuziki

0
513
Peter Msechu

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na ngoma zake kama vile Relax na Nyota, Peter Msechu amekanusha tetesi za kushuka kimuziki.

Tetesi za Peter Msechu kufulia zilitokana na ukimya wake Kwenye gemu kwa kipindi kirefu bila ya kuwa na nyimbo iliyofanya vizuri kwa muda mrefu kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Peter Msechu amesema kwa sasa anaimarisha shughuli zake za ujasiriamali ambazo zinamuingizia kipato kikubwa cha kuandaa sherehe, kupamba maharusi na shughuli mbalimbali za kijamii.

Peter Msechu ameweka wazi kuwa kwa sasa anafanya muziki jitihada zake amezielekeza Kwenye biashara zake zitakazoweza kumuingizia kipato kikubwa kitakachoweza kumkwamua kimaisha.

LEAVE A REPLY