Msechu afanya mazoezi kupunguza mwili wake

0
21

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu amesema kuwa pamoja na kufanya mazoezi ya kupunguza unene ila hatathubutu kupunguza tumbo lake kwa kuwa ndio utambulisho wake.

Peter Msechu amesema mabadiliko hayawezi kuonekana mapema kama mtu hafuatilii kwa makini kwa kuwa ameanza mazoezi tangu mwezi Machi mwaka uliopita.

Amesema alikuwa na kilo 132 ila kwa sasa ana kilo mia moja na kumi na watu hawajui kuwa anafanya mazoezi kwa afya lakini kitu ambacho hatoweza kupunguza ni tumbo lake na wala hafanyi mazoezi ili kupunguza tumbo.

Hata hivyo amemaliza kwa kusema kuwa harusi yake atafunga baada ya miaka mitano kwa kuwa anasubiri pete aliyomvisha mpenzi wake ichakae ndio maana amekuwa kimya na anafikirii kumuoa mpenzi wake huyo.

Pia amesema kuwa baada ya miaka mitano kwa kuwa tayari ameshakaa nae kwa miaka sita, hivyo ndani ya miaka hiyo sita kwake yeye ni kama ndoa na harusi yake anataka ifungwe kwenye maji.

LEAVE A REPLY