Msando achaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Hakimiliki

0
91

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amemchagua Mwanasheria na mdau wa masuala ya Sanaa Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Katika tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Kwa upande wa Alberto Msando ambaye amepatiwa nafasi hiyo na serikali ameahidi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

Msando ameandika  “Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya ‘naomba nitoe niko vibaya’. ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii”.

Ameongeza “Harrison Mwakyembe tutafanya kazi uliyotutuma”

Msando mara nyingi amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria.

LEAVE A REPLY