Msamii amwagia sifa mama mtoto wake

0
57

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami amesema kuwa msimu huu wa siku ya wapendanayo anatarajia kurudisha mapenzi kwa mpenzi wake kwani amekuwa mwanamke bora kwake.

Ametoa kauli hiyo kuelekea sikukuu ya wapendao itakayofanyika siku ya Alhamisi ambapo wapenzi watahadhimisha upendo wao.

Msanii huyo amedai kuwa muda mwingi anawaza kurudisha mapenzi kwa mama wa watoto wake kwa sababu amekuwa mama bora kwa mtoto wake lakini mwenye uvumilivu sana kwake.

Msami amesema kuwa pamoja na kwamba kuna muda anakuwa mbali nae lakini amekuwa akimjali na kuheshimu sana hisia zake na kazi zake pia, anasema kuwa mama huyo ni mwanamke anaeamini kuwa anampenda kutokana na mapenzi yake.

Sikukuu ya wapendanao inawaleta wapandanao pamoja kwa ajili ya kusheherekea pamoja na kudumisha mapenzi yao maishani.

LEAVE A REPLY