Msami ahaidi kumsaidi mshindi wa Ishi Kistaa Valentine’s Day aliyekimbiwa na “Mumewe”

0
146

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami akiwa na mshindi wa Ishi Kista Valentine’s Day aitwae Flora ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

Katika maongezi yao mama huyo alimuadithia Msami kuhusu kuachiwa mtoto na mwanaume aliyezaa nae.

Mama huyo ameanza kwa kutoa stori yake fupi ‘kuwa alikuwa anaishi na mwanaume wake maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam na wakabarikiwa kupata mtoto mmoja’.

Mama huyi akaendelea kusema kuwa ‘Baada ya kujifungua mtoto wa kike anayeitwa Linah mwanaume wake akaanza kubadilika na kuanza kumpiga kila wakati anaporudi nyumbani lakini akavumilia.

Mama huyo akaendelea ‘kusema kuwa kuna siku mwanaume wake akampa nauli shilingi elfu 10 ili aende kwao maeneo ya Mbande kwa ajili ya kusalimia wazazi wake’.

Akaendelea kusema kuwa wakati aliporudi nyumbani kwa mumewe huyo akakuta ameahama na kuhamisha kila kitu akimpigia simu anamwambia yupo mkoani Tanga na hatorudi tena Dar es Salaam.

Mama huyo kwasasa anaishi kwao Mbane ambapo anamlea mwanawe peke yake bila matunzo yoyote (child support) kutoka kwa baba.

Baada ya kupewa stori hiyo fupi Msami ameonesha kuguswa na tatizo la mwanamke huyo ambapo ameahidi kumsadia kwa ajili ya malezi ya mtoto wake.

LEAVE A REPLY