Msami afunguka Ruge alivyomsaidia kimaisha

0
47

Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Msami amefunguka na kuweka wazi Jinsi Marehemu Ruge Mutahaba alivyomsaidia na kumtoa kwenye maisha ya wizi.

Msami alisema kipindi hicho alikuwa akiishi maisha ya kihuni Temeke ambapo alikuwa mwizi wa kutupwa na tena wa kuvunja nyumba za watu, kuiba mali na kwenda kuuza lakini anamshukuru sana Ruge ndiyo ameweza kuona kipaji chake na kumwambia aachane na hivyo vitu aimbe.

Nitalia siku zote juu ya Ruge, ameniepusha na kifo mimi maana jamaa niliyekuwa naiba naye majumbani kwa watu aliuawa.

 Pia Msami ameweka wazi kuwa moja ya mafanikio makubwa aliyokuwa nayo ni Ruge kumuamini kuwa msanii na kiongozi wa madansa na pia kumfanikishia kununua gari aina ya Toyota IST (nyeusi) ambayo imekuwa ikim-saidia katika kazi zake za kimuziki.

LEAVE A REPLY