Msako mkali kuwabaini ‘wahaini’ wa serikali ya Zimbabwe waanza

0
170
 Waziri wa ulinzi wa Zimbabwe, Sydney Skeremayi amelaani kitendo cha chama cha wanajeshi maveterani cha kuacha kumunga mkono rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.
 Chama cha wanajeshi wastaafu wa Zimbabwe (Zimbabwe National Liberation War Veterans’ Association) kilitangaza wiki iliyopita kuwa hakitamuunga mkono rais Mugabe kwenye uendeshaji wa serikali kwasababu ni mjivuni na anaongoza vibaya.
Kwenye taarifa yake, waziri Skeremayi ameyaita maandamano ya wiki iliyopita yaliyofanywa na wanachama wa chama hicho kuwa ni alama ya ‘uhaini’ kwa serilai ya nchi hiyo.
 Wastaafu hao ambao walishirikiana na rais Mugabe kupigana vita kwaajili ya kulikomboa taifa hilo kutoka kwenye utawala wa kikoloni, walifanya maandamano yao kwenye mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Waziri Sydney Skeremayi amedai kuwa taarifa ya umoja huo waliyoitoa kwenye maandamano ya wiki iliyopita iliandaliwa na aliowaita ‘fifth column’ jina ambalo hutumiwa kukitaja kikundi cha wanachama ndani ya chama hicho ambacho kinadaiwa kuhadaa na kukwamisha chama cha maveterani hao.

 

Gazeti la serikali la The Herald limedai kuwa tayari serikali ya nchi hiyo imeanzisha uchunguzi kubaini watu wanaohusika na kile walichokiita ‘uhaini’.

waziri

LEAVE A REPLY