Mrisho Mpoto amtaka Steve Nyerere kuacha kuponda tuzo za Sinema Zetu

0
180

Mwanamuziki wa nyimbo za asili nchini, Mrisho Mpoto amemjibu muigizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere baada muigizaji huyo kuponda utoaji wa tuzo za Sinema Zetu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mpoto ameandika ‘Steve Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele, nikahisi tofauti kidogo: Kwakua kilikua kipindi cha jua kali kidogo.

Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na Filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa….ya uigizaji…

Zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga…siyo lazima apewe unaemtaka wewe Stive. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa.

LEAVE A REPLY