Mrembo wa Kenya ashinda taji la miss Afrika

0
212

Shindano la malkia wa urembo duniani la 2017 lilikamilika mjini Sanya China siku ya Jumamosi huku Mkenya Magline Jeruto akishinda taji la malkia wa urembo barani Afrika.

Hatua hiyo inajiri baada ya mwanadada huyo kutoka eneo la Elgeyo Marakwet nchini Kenya kuchukua nafasi ya tano.

Taji la malkia wa urembo duniani lilichukuliwa na mwanadada wa India Manushi Chhillar.

Andrea Meza wa Mexico alichukuwa nafasi ya pili akifuatiwa na Muingereza Stephanie Hill huku naye Aurore Kichenin wa Ufaransa akishinda nafasi ya nne.

Haki miliki ya picha facebook/Jeruto Image caption Magline Jeruto ndiye mshindi mpya wa taji la malkia wa Urembo barani Afrika

Magline Jeruto ambaye ndiye malkia wa urembo wa Elgeyo Marakwet alichukua nafasi ya tano miongoni mwa wagombea 118 katika shindano la malkia mrembo dunia.

Mwanadada mwengine wa Afrika ambaye aliorodheshwa katika nafasi kumi bora ni Ade van Heerden wa Afrika Kusini ambaye alimaliza katika nafasi ya tisa.

LEAVE A REPLY