Mrembo wa Kenya akanusha kuolewa na Alikiba

0
357

Video vixen kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anatarajia kufunga ndoa na mwanamuziki Alikiba.

 

Mrembo huyo ameamua kuweka wazi suala hilo baada ya habari hizo kusambaa katika mitandao mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kuhusiana na ndoa ya wawili hao kutarajiwa kufungwa hivi karibuni.

 

Kupitia mtandao wa Snapchart mrembo amekanusha kwa kusema kuwa yeye na Alikiba walifanya kazi kwenye video ya Nagharamia ambayo Alikiba alifanya na mwanamuziki, Christian Bella baada ya hapo hakuwa na mawasiliano naye tena.


Tanasha amekana taarifa hizo ikiwa ni wiki moja kupita tokea ripoti idai kuwa wawili hao wanamatarajio ya kufunga ndoa.

 

Taarifa za Alikiba na mrembo huyo kufunga ndao zimezagaa katika mitandao ya kijamii hapa nchini kabla ya mrembo huo kukanusha vikali taarifa hizo.

LEAVE A REPLY