Mr Nice amchana Dudu Baya

0
218

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr Nice amejibu tuhuma za msanii mwenzake Dubu Baya aliposema kwamba maisha yamemshinda na kukimbilia Kenya.

Mr Nice amesema kuw Dudu Baya ni msanii asiyejielewa, ndio maana hana mahali pa kuishi licha ya kuwa maarufu.

Mr.Nice amesema ni wakati sasa Dudu Baya akomae na game kama anavyofanya yeye, kwani muda wa malumbano na kuchafuana hautamsaidia chochote, na hastahili kufanya hayo kwakuwa umri umeshamucha.

Mr. Nice ameendelea kwa kusema kwamba Dudu Baya ni mlevi na anaishi maisha ya kuigiza, hivyo kabla hajaanza kumuongelea vibaya ni vyema akaanza kujilinganisha naye kama wanafanana kimaisha.

LEAVE A REPLY