Mr Blue athibitisha kupata mtoto wa tatu

0
37

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Mr Blue amejaliwa kupata mtoto wa tatu wa kike na mke wake Waheeda aliyejifungua hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Mr Blue amethibitisha hayo kupitia post yake aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram amehabarisha kuwa amepata mtoto mwingine na mkewe Waheeda.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Ahsante mke wangu Mrs Blue Beauty Cosmetics kwa zawadi nyingine alhamdulillah, ahsante sana Mungu kwa kheri zako, karibu sana binti yangu Khairat kwenye familia alhamdulillah, Mungu ni mwema sana”.

Ni mtoto wa tatu kwa msanii huyo na mkewe kwani hapo awali walikuwa na watoto wawili ambao mmoja wakiume mwingine ni mtoto wa kike.

LEAVE A REPLY